Msanii Gully Gad, aka Mavado kutokea Jamaica anayefanya muziki wa Dance hall ameshambuliwa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii baada ya kujivisha uhusika na kujifanya Yesu katika moja ya picha alizoweka katika ukurasa wake mapema wiki hii.

Msanii huyo wa Dancehall ametumia ukurasa wake wa instagram kupost picha hiyo na wengi kudai kuwa kitendo cha kupiga picha hiyo ni kwaajili ya kuitumia katika project yake ijayo ya muziki.

Kutokana na picha hiyo mashabiki wengi hasa wakristo wamemjia juu kumkosoa na wengi kusema kuwa anavunja sheria pamoja na kuikosea heshima dini ya Kikristu, na wengine kumtaka asimchukulie Yesu kwenye masuala ya utani, wakionesha kuchukizwa na kitendo hicho wameushambulia ukurasa wake kwa kumkosoa .

“Mavado Mimi ni shabiki mkubwa lakini hii picha hapa sio sahihi kwangu mimi kama mwanamke mwenye kuogopa Mungu, tafadhali,”

msichana mmoja aliandika

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here