Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Mussa Hussein amemshauri, msanii wa Injili, Joel Lwaga kubadilika na kuwafuata watu wengine wasioamini hasa kwenye mabaa ili waamini na kumfuata Mungu na yale anayoyaimba kwenye nyimbo zake za Injili.

Mussa Ametoa ushauri huo wakati msanii huyo alipokuwa akitambulisha wimbo wake mpya uitwao Umejua Kunifurahisha kwenye kipindi hicho.

‘’Ukijifunza maisha ya Bwana Yesu alikuwa akijaribu kuwachukua wale wasioamini ili waamini, kwahiyo ni wakati sasa wa kuwachukua wengine ambao hawapo ili kuwaleta kwa Bwana, kila siku mnapiga makanisani nataka siku moja uwende pale Kona Bar ukawaimbie’’

Alisema Mussa Hussein.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here