Kuwepo kwa matamasha na ibada mbalimbali za kusifu na kuabudu imekuwa ni moja kati ya tamaduni zinazokuwa kwa haraka Zaidi huku utaratibu huu ukionesha matokeo chanya kwa kuwavuta vijana wengi sana pindi mikesha na matamasha ya nanmna hii yanapotokea.

Mchungaji Godsave Sakafu pamoja na mkewe wameandaa mkesha mjini Arusha chini ya kanisa la Victory Christian Centre international (VCCI), mkesha huo utahusisha waimbaji mbalimbali wa kimataifa pamoja na waimbaji wa ndani pamoja na wanenaji mbalimbali maarufu.

Katika kuhakikisha hilo mchungaji Godsave pamoja na mkewe Angel Bernad ambaye ni muimbaji mkubwa nchini Tanzania wamekuwa wakitumia akaunti zao kuwahabarisha na kuweka matangazo kila habari mpya inapotokea, katika kurasa zao moja ya Tangazo limesomeka hivi.

Ule mkesha mkubwa🙌 na wa kihistoria kuwahi kutokea katika jiji la Arusha ni tarehe 09.11.2018🔥 Jiji zima la Arusha, Kilimanjaro na mikoa mingine ya karibu Watu wote tunakutanika katika uwanja wa sheikh amri abed mapema tu kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 12:00 asubuhi. Tutamsifu Mungu na kumwabudu🎶🙏Mungu pamoja na kujifunza Tutakuwa na Mkhululi Bhebhe mwimbaji wa wimbo wa tambira Jehovah kutoka joyous celebration South Africa, Joel Lwaga, Dr Ipyiana Kibona, Adownage kutoka Kenya, Emmanuel kutoka Zambia, Justine kutoka Rwanda, shwangwe voices, Eliya mwantondo, Jay johnas Machalii wa Yesu na Jamrack. Wanenaji 🎤 ni Bishop Deo Lubala, Dr Ringo mowo, Samweli Ndandala, Joel Nanauka & pst Godsave. Entrance :college students 3000/= Others. 5000/= Dj music DJ Sam. Food, drinks and snacks will be available at your own cost🍹🍔. Hosted by Victory Christian Centre international (VCCI) under Pst Godsave &Angel Sakafu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here