Joel Lwaga

Utambulisho.

Joel Lwaga ni muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, muabudu halisi aliyeitwa kuleta Tumaini.
Pia ni Msomi mwenye Shahada ya Uchumi, mwandishi wa nyimbo na mwalimu wa Sauti.

Historia Fupi.

Kama ilivyo kawaida ya waimbaji wengi kuanza kujifunza kuimba wakiwa na umri mdogo ndivyo hivyo ilivyokuwa kwa muimbaji huyu, ameweka wazi kuwa alianza kuwa na mapenzi na muziki akiwa na umri mdogo kabisa kwenye shule ya Jumapili ya watoto yaani “Sunday School” na baadaye kujiunga na kwaya ya vijana akiwa kama muimbaji na mwalimu wa kwaya hiyo wakati huo akiwa anasali katika kanisa la Morovian kabla ya kuhamia Tanzania Assemblies of God (TAG) ambapo kwa mara ya kwanza alijiunga na Kanisa la City Christian Center lililopo Upanga Jijini Dar es salaam.

ulimwengu wa uimbaji nchini Tanzania ulianza kufunguka kwa muimbji huyu Mwaka 2013 ambapo alipata nafasi ya kuongoza sifa na kuabudu kwenye ibada kubwa ya AFLEWO (Africa Let’s Worship) pamoja na AFLEWO Mass Choir ya Dar es Salaam ibada ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka katika nchi mbalimbali Barani Afrika, na kuhudhuliwa na wakristo wa makanisa tofauti tofauti kwa lengo la kumsifu Mungu kumtukuza na kumuomba kwa Pamoja..

Baada ya hapo, Joel alijiunga na kundi la Glorious Worship Team huku akiendelea kuhudumu kanisani kwake ndani ya kundi la The Next Level team.

Akiwa GWT alifanikiwa kushiriki kwenye albam ya kundi hilo inayojulikana kama “Waweza” ambapo katika albam hiyo aliweza kutunga na kuongoza wimbo uliobeba albam “Waweza” na wimbo mwingine unaoitwa “Ameniona” kabla ya kuachana na kundi hilo, ambalo alidumu nalo kwa muda wa miaka miwili.

Punde Joel alianza kuimba kama muimbaji binafsi na kuweka wazi kuwa hakutoka ndani ya kundi kwa ubaya wowote bali ni suala la majira, nyakati na maono.

Kuimba kama Muimbaji Binafsi

baada ya kumaliza Elimu yake chuoni Joel aliingia rasmi katika utumishi akidhamilia kuweka Muda wake wote katika kumtumikia Mungu, kitendo ambacho kilimpa nafasi ya kutembelea majiji mbalimbali na baadae kutembelea nchi kadhaa akimtangaza Mungu kwa njia ya Uimbaji.

Mapema mwaka 2017, Joel Lwanga alitoa wimbo wa Sitabaki kama nilivyo Wimbo ambao uligusa maisha ya wengi na Kumuweka katika orodha ya waimbaji Nyota wa Nyimbo za injili nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Ukubwa wa wimbo ulifuatiwa wa Album yake kama muimbaji binafsi  SITABAKI KAMA NILIVYO ambao umempa umaarufu zaidi, Joel Lwaga ameendelea kuachia nyimbo zilizopo kwenye albam yake hiyo kadri muda unavyozidi kwenda zikiwa kwa mfumo wa video.

kama vile haitoshi amezidi kuleta matumaini makubwa baada ya kuachia wimbo aliofanya na muimbaji kutoka nigeria Umejua Kunifurahisha rekodi ambayo imefanya wengi kutabiria mafanikio makubwa katika safari yake ya uimbaji
mpaka hivi sasa Joel Lwaga ana Album moja SITABAKI KAMA NILIVYO inapatikana YouTube kwa baadhi ya nyimbo lakini unaweza download nyimbo zake kupitia boomplay.

Contacts
Instagram- @joellwaga_official
Facebook- @Joel Lwaga

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here