Mwimbaji wa Gospel, Joel Lwaga amekanusha vikali kuhusiana na uvumi unaovuma kuwa amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanadada Muna Love.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari maarufu  nchini Tanzania kuhusu uvumi huo wa mitandaoni, muimbaji huyo alisema hayuko tayari kulizungumzia kwani halihusiani kabisa na huduma yake yeye kama mtumishi wa Bwana. Na kuongezea kuwa hawezi kuzuia mtu au kikundi cha watu kuandika kumuhusu yeye.

‘’Mimi ni Mtumishi wa Mungu, ningekuwa nimechumbia ingekuwa wazi, siwezi kuchumbia kimya kimya. Mimi si mtu gizani ni wa rohoni wakati ukifika wa kuchumbia kila mtu atajua, sijawahi kuwa na mchumba’’

Alisema Joel Lwaga.

’Huwezi kuzuia mtu kuandika anachojisikia siwezi kujibu walichoandika, najibu kutokana na uhalisia ulivyo wakati ukifika wa kuwa na mchumba watu watafahamu’’ Aliongeza Joel Lwaga.

Joel Lwaga hivi sasa anatamba na wimbo wake wa “umejua kunifurahisha “ alioshirikiana na muimbaji wa Gospo kutoka Nigeria Chriss shalom, wimbo ambao umevunja rekodi kati ya nyimbo alizowahi kufanya Joel kwa kuangaliwa na watu wengi sana kwa muda mchache katika mtandao wa Youtube.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here