Msanii wa nyimbo za injili nchini ,Emanuel Mbasha amekuwa akiongea na kulalamika kwa uchungu sana tangu alipoachana kwa talaka na mzazi mwenzie Florah Mbasha miaka minne iliyopita  baada ya mwanamke huyo kumkatalia mtoto aliewahinkuzaa nae walipokuwa katika ndoa.

Emmanuel anasema kuwa kwa takribani miaka minne sasa hajawahi kuonana na mtoto wake na hata pich ya mwisho aliyokuwa nayo ya mtoto huyo ni ile aliyopiga nae siku ya mwisho walipokuwa mahakamani kufuatilia talaka.
Emmanuel anasema kuwa inazidi kumuumiza kwa sababu ndio mtoto pekee aliyenae aliempata akiwa kijana lakini alimlea kwa mapenzi tangu alipozaliwa akiwa mchanga na yeye ndio alikuwa akimlea mtoto huyo.
“Unajua Liz ni mtoto wangu wa ujanani, nimemlea tangu akiwa mchanga kabisaa, mara ya mwisho kumuona  ni pale mahakamani mwaka 2014 tulipopeana talaka na mama yake  na nikapiga nae picha na baada ya hapo mama yake amekuwa akimkatalia  nisimuone kwaio imekuwa changamoto sana kwangu”.
Mbasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here