Muimbaji mkongwe kutoka Tanzania na mshindi wa tuzo mbalimbali za kimataifa kupitia muziki wa injili Rose Muhando ameingia tena kwenye vichwa vya habari baada ya kujiita simba siku chache tu baada ya video yake akiombewa iliyozua Gumzo mtaani.

Video hiyo iliyomuonesha Muimbaji huyo akitolewa mapepo na mchungaji James Ng’ang’a wa Evangelism Center nchini Kenya ilisambaa mitandaoni na kuzua mijadala mbalimbali huku kila mmoja akitoa maoni yake kuhusu video hiyo fupi.

Jumatano iliyopita katika tamasha alilohudumu akiwa na Stephen Kasolo Rose Muhando alipata nafasi ya kuzungumza machache na alikaliliwa akisema yeye ni simba.

“I have gone through a lot. The hardships have given me a chance to build endurance, hence the reason you can call me Lioness,”

kwa tafsiri isiyo rasmi alimaanisha kuwa amemepitia mengi. na hayo aliyopitia yamejenga uvumilivu wake hiyo ni sababu inayotosha kumuita Simba

“kazi yangu ni kuwinda, siogopeshwi na chochote, ninapo unguruma, kunawatu wanapata pigo, na sitachoka mpaka Utukufu wote anapewa Mungu wangu.“

aliongezea Rose Muhando.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here